Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ameahidi kutoa Shilingi laki tano kwenye mshahara wake wa mwezi wa kwanza na wa pili kwa mwaka 2019 kwa ajili ya Baraza la wafanyakazi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru ili zisaidie katika kuibua masuala ya maendeleo huku akisema ana miezi mitatu hajapumzika kwa kufanya kazi.
DC Muro amesema ndani ya miezi mitatu hiyo amefanya kazi ambayo ingefanywa kwa mwaka na amefanya hivyo ili kuhakikisha Rais atakapofika Arumeru asikute lawama za wananchi.
UTEUZI: Mkurugenzi Mkuu mpya wa NHC ateuliwa