Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga inaendelea tena wikendi hii na mechi ambayo itaangaliwa na macho ya wengi ni RB Leipzig dhidi ya Hertha Berlin, RB Leipzig wako katika kiwango bora lakini wakiwa wamelingana point sawa na Hertha Berlin tofauti ikiwa ni magoli ya kufunga na kufungwa.
Weekend hii Ligi Kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga kuna michezo mingi inachezwa miongoni mwa michezo hiyo ambayo itakuwa ya kuvutia sana ni ule wa RB Leipzig dhidi ya Hertha Berlin, huku RB Leipzig ikitamba na mshambuliaji wao wa Denmark mwenye asili ya Tanzania Yussuf Poulsen.
Leipzig hawajashuka sana ukilinganisha na kiwango walichokuwa nacho msimu uliopita, Hertha Berlin pia wana msimu mzuri hadi sasa ikiwa ni tofauti tu ya magoli ndio inawatofautisha na Leipzig ambao wako nafasi ya tano kaatika msimamo wa ligi.
Hertha Berlin kwa sasa wanatamba na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Salomon Kalou ambaye amezidi kudhihirish kuwa umri ni namba tu, wiki iliyopita alifunga mabao mawili katika droo dhidi ya vinara wa ligi hiyo Borussia Dortmund. Kalou anatarajiwa kuwa tishio tena katika mchezo huo wa wikendi hii.
Mchezo huu utakuwa moja kwa moja kupitia chaneli ya ST World Football ndani ya king’amuzi cha StarTimes tena kwa lugha ya Kiswahili, kuanzia saa 2: 30 Usiku Jumamosi ya Novemba 3.
Game nyingine za Bundesligai zinachezwa ni pamoja na hii ya FC Bayern Munich vs Freiburg saa 11: 30 jioni, Schalke vs Hannover, Bayern Leverkusen vs Hoffenheim, Wolfsburg vs Borussia Dortmund na siku ya Jumapili ni Borussia Monchengladbach vs Dusseldorf na Mainz vs Werder Bremen game hizo zitaoneshwa na StarTimes.
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19