Leo Novemba 5,2018 nakuletea stori hii kutoka katika Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambapo Ubalozi huo umewaonya Raia wake wanaoishi Tanzania kuchukua tahadhari juu ya kampeni ya mkuu wa Mkoa wa DSM ya kuwakamata na kuwashtaki Watu wanaojihusuisha na ‘Ushoga’.
Ubalozi huo umewashauri Raia wake kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii kuondoa lugha ama picha zinazoweza kuhusishwa na ‘Ushoga’ kwani ni kinyume na sheria za Tanzania.
Onyo hilo ambalo limetolewa kupitia tovuti ya Ubalozi huo limewataka pia Raia wa Marekani kuhakikisha kwamba Maafisa wa Tanzania wanawajulisha kukamatwa ama kuzuiliwa kwao.
Mkuu wa Mkoa wa DSM aliteua kamati maalumu kwa ajili ya kuwatambua Watu wanaojihusisha na ‘Ushoga’ na kuhakikisha wanafikishwa katika vyombo vya sheria.