Baada ya kuwepo kwa taarifa kuhusiana na kukamatwa kwa wanaharakati wawili wa kamati maalumu ya kuwalinda wanahabari duniani (CPJ), leo November 8 2018 Idara wa uhamiaji imethibitisha kwamba mnamo November 7 2018 wanaharakati iliwakamata wnaharakati hao.
Taarifa kutoka idara ya uhamiaji zimeeleza kuwa wageni hao waliomba na kupatiwa kibali cha matembezi cha miezi mitatu ambacho kinaisha muda wake January 1 2019. Baada ya mahojianio walikiri kuwa wameingia nchini kwa kwa lengo la kufanya vikao na waandishi wa habari nchini wakati vibali vyao ni kwa ajili ya matembezi ambapo ni kinyume na sheria ya uhamiaji.
Hata hivyo baada ya uchunguzi idara ya uhamiaji imewaachia huru na kuwarejeshea pasipoti zao kwa masharti ya kutoendelea na vikao hivyo kwa kutumia vibali vya matembezi walivyopewa. Unaweza kubonyea hapa chini kusikiliza kila alichozungumza msemaji wa Idara ya Uhamiaji kwa kubonyeza play hapa chini
‘Baada ya kuona Waziri Kairuki alinipigia simu’-Abdul Nondo, Bonyeza play hapa chibi kutazama