Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo usiku wa saa 3 kwa saa za Afrika Mashariki inaingia uwanjani huko Windhoek kupambana na timu ya taifa ya Namibia katika mchezo wa kirafiki.
Kocha wa timu hiyo Salum Madadi ametangaza kikosi cha Stars kitakachoanza leo
Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Hassan Banda, Aggrey Morris, Said Morad, Himid Mao, Ramadhan Singano, Jonas Mkude, Juma Luizio, Amri Kiemba na Haruna Chanongo.
Wachezaji wa akiba ni Shaban Hassan Shabaan ‘Kado’ Michael Pius, Hamis Mcha na Athanas Mdamu.