Kuna msemo usemao mashabiki wa mchezo wa soka wana mapenzi ya wazimu kwa wachezaji au timu wazipendazo.
Msemo huu umepata mfano sahihi baada ya shabiki mkubwa wa Liverpool ambaye ni baba wa mchezaji wa beki wa timu ya taifa ya Denmark, Simon Kjaer, amempa amri mtoto wake Simon Kjaer kuomba jezi ya mchezaji wa England Steven Gerrard baada ya mchezo wa kirafiki baina ya England na Denmark.
Simon Kjaer ambaye anaichezea klabu ya Lille ya Ufaransa amesema familia yake nzima ni washabiki wa Liverpool, na baba yake alipogundua Denmark itacheza mechi ya kirafiki na England akampa amri mwanae arudi na jezi ya Gerrard baada ya mchezo huo.
“Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu ya soka itanibidi nimfuate mchezaji mwingine na kumuomba jezi yake – na hilo ni jambo la aibu kiasi.’