Usiku wa November 10 2018 mchezo wenye mvuto zaidi ndani ya Ligi Kuu Ujerumani kati ya Borussia Dortmund dhidi ya FC Bayern Munich ulichezwa katika uwanja wa Signa Iduna Park, huu ni mchezo wa 11 wa Ligi Ujerumani kwa timu zote mbili msimu huu lakini mvuto wa mchezo huu unakuja pale Dortmund anapokuwa nyumbani halafu hana rekodi nzuri dhidi ya Bayern Munich.
Dortmund akimkaribisha FC Bayern Munich katika uwanja wake wa Signal Iduna Park amefanikiwa kuushangaza ulimwengu wa soka kwa kupata ushindi wa magoli 3-2 licha ya kutanguliwa kufungwa mara mbili, FC Bayern Munich walipata goli dakika ya 26 kupitia kwa Robert Lewandowski lakini Dortmund wakasawazisha kwa penati dakik ya 49 kupitia kwa Marco Reus kabla ya Lewandowski kufunga tena la pili dakika ya 53.
Borussia Dortmund ikiwa rekodi haiwabebi kwa miaka ya hivi karibuni dhidi ya Bayern walifunga goli la kusawazisha tena dakika ya 67 kupitia kwa yule yule Marco Reus kabla ya Alcacer kuhitimisha ushindi wa Borussia Dortmund dakika ya 73 kwa goli maridadi, ushindi huo unawafanya FC Bayern kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Bundesliga kwa point 27.
Katika game 11 za Bundesliga Dortmund kashinda game nane sare tatu na hawajapoteza mchezo wakati Bayern wapo nafasi ya 4, kwa kubaki na point zao 20, wakishinda game 6, sare 2 na wamepoteza game ya tatu leo hii, ushindi wa Dortmund kwa FC Bayern ndani ya Bundesliga unakuja kwa mara ya kwanza baada ya siku 719, Dortmund mara ya mwisho kumfunga Bayern ndani ya Bundesliga ilikuwa November 19 2016.
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19