Hadija ni kondakta wa magari madogo (Daladala) kutoka stand ya Kilombero hadi Moshono Arusha ambaye ameanza kazi miaka mitano iliyopita na ameweza kuwasomesha watoto wake hadi Sekondari kutokana na fedha anayoipata na hajawahi kuajiriwa bali anaaminiana na madereva kutokana na utendaji wake wa kazi.
Changamoto anayokutana nayo mara nyingi huwa ni kutongozwa na baadhi ya watu anaokutana nao akiwa kazini.