Shirikisho la soka Tanzania TFF kwa kushirikiana na wadhamini wakuu wa michuano ya SportPesa Super Cup, wameamua kuyaboresha mashindano hayo kwa kuyaweka kwenye kalenda yao ya TFF.
TFF imeyaweka mashindano hayo kwenye ratiba ya michuano ya TFF ili kuondoa changamoto kwa wachezaji wa vilabu shiriki kwani yalikuwa yanaingiliana na likizo, hivyo sasa yameboreshwa na mwaka 2019 yatachezwa kuanzia January 22 kwa kutumia viwanja vya CCM Kirumba Mwanza na Dar es salaam.
Michuano hii Bingwa atapewa zawadi ya dola 30000 sambamba na kupata nafasi ya kucheza mechi ya kirafiki na Everton katika uwanja wa nyunbani wa timu Bingwa wa michuano hiyo.
Mwaka 2019 michuano hiyo itashirikisha timu kutoka mataifa mawili kama ilivyo kawaida yake Kenya na Tanzania na kwa upande wa Tanzania, timu shiriki ni Simba SC, Yanga SC, Singida United na Mbao FC ambaye amealikwa na wadhamini wakuu SportPesa ili kuleta chachu ya mashindano hayo.
Kwa upande wa Kenya timu za Gor Mahia ambaye ndio Bingwa mtetezi wa michuano hiyo atashiriki, AFC Leopards, Bandari ya Mombasa na Kariobangi Sharks.