Baada ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Luoga kusema kwamba walitumia Wanajeshi kwenye oparesheni ya safishasafisha kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni Arusha kutokana na upungufu wa Polisi, Mbunge wa Arusha Mjini ameita Waandishi kulizungumzia hilo.
Lema amesema “Arusha mjini shule zilizopo za Sekondari zilizokua zinafanya Mtihani ni 24 kati ya 25 maana yake ni dhahiri kama Arusha kama Mkoa walikua na Polisi wa kutosha kabisa kufanya hii Oparesheni, Polisi walikuwepo wa kutosha….“
“Mbinu iliyotumiwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa kazi ambayo walikua wanataka kuifanya ni mbinu mbaya japokua nia inaweza kuwa ilikua ni nia njema kabisa, wangeweza kabisakabisa kuifanya na Polisi ama TAKUKURU na swala hili lingekwenda kiulaini bila kutengeneza tension kwa Wafanyabiashara wenyewe, Watu na Jamii za kimataifa”
.