Leo November 26, 2018 Upelelezi kesi ya uchochezi inayomkabili, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Zitto anatarajia kusomewa maelezo ya awali (Ph) December 13,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amemueleza Hakimu Shaidi kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na anaomba tarehe kwa ajili ya (Ph).
Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi December 13,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).
Katika kesi hiyo Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi ambapo anadaiwa ametenda October 28, 2018 katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo.
Pia anadaiwa October 28, 2018 huko Kijitonyama Kinondoni katika mkutano huo na Wanahabari, Kabwe alitoa maneno ya uchochezi. Zitto yupo nje kwa dhamana.
AMBER RUTTY ANAO WADHAMINI WAWILI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
DAKIKA 240, SHOW YA ALIKIBA KAHAMA, NI BAADA YA MVUA KUBWA. BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA