Leo November 28, 2018 Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Sam Rumanyika amelazimika kupiga simu akiwa ndani ya chumba cha Mahakama na kuzungumza karani wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati wa Rufaa ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Jaji Rumanyika amefanya uamuzi huo baada ya Wakili wa Mbowe na Matiko, Peter Kibatala kudai kuwa nyaraka za uamuzi wa kesi ya warufani hao can kutokea Mahakama ya Kisutu hazionekani.
Baada ya kueleza hayo Jaji Rumanyika aliomba apewe namba za Karani wa Kisutu ili aweze kumpigia simu akiwa ndani ya chumba cha mahakama.
Jaji Rumanyika alimpigia simu Karani huyo na kuweka Loud Speaker, ambapo alijitambulisha kuwa yeye anaitwa Rumanyika yupo Mahakama Kuu na anaulizia kwanini nyaraka za uamuzi wa mwenendo wa kesi ya Mbowe na wenzake hazijakamilika.
Karani huyo alijibu kuwa ni kweli anaifahamu kesi hiyo na nyaraka nyingine zinaendelea kuchapwa, hivyo hazijakamilika.
“UKIKUTWA UCHOCHORONI NA MWANAFUNZI WA KIKE, UNA ADHABU YAKO” WAZIRI MKUU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA