Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 23 anayecheza soka katika club ya Singida United Habib Haji Kyombo, leo ameripotiwa kufuzu vipimo vya afya vya kujiunga na club ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Kupitia ukurasa wa instagram wa ShadakaSports Managent wanaojihusisha na usimamizi wa wachezaji na uongozi katika michezo, wametibitisha taarifa hizo za mteja wao kufanikiwa kufuzu vipimo vya afya na sasa yanasubiriwa makubaliano binafsi kati ya club na mchezaji ili asaini.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Habib Haji Kyombo aliyekuwa tishio katika kufumania nyavu, alijiunga na Singida United akitokea Mbao FC ya Mwanza mapema mwaka huu, kama Habib atafanikiwa kusaini mkataba atakuwa anaungana na mtanzania mwenzake Abdi Banda katika Ligi moja ya Afrika Kusini, Banda akiichezea Baroka FC.
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?