Azam FC leo Jumanne ya December 4 2018 walikuwa katika uwanja wao wa Azam Complex Mbande Chamazi kuwakaribisha Stand United ya Shinyanga, Azam FC wakiwa katika uwanja huo walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1, hiyo ni baada ya kutokea nyuma baada ya Stand kupata goli la uongozi dakika ya 53 kupitia kwa Hafidh Musa.
Kocha Mkuu wa Azam FC Hans van Pluijm alifanikiwa kubadili mchezo baada ya kufanya mabadiliko ya kumuingiza Yahya Zayd aliyefunga magoli mawili dakika ya 72 kwa penati na dakika ya 85, Yahya alikuwa na mchango zaid kwani alifanikiwa kutoa assist ya goli la kwanza la Azam FC dakika ya 66 lililofungwa na Enock Atta, hivyo baada ya mchezo Zayd alieleza kitu kilichomfanya vizuri akitokea benchi ni kuusoma mchezo tu.
“Mimi namshukuru Mungu sababu bila yeye nisingeweza kufanya hiki kilichoonekana leo kingine niongezee ni juhudi za wachezaji wote, tulioweza kushirikiana ndio tumeweza kupata matokeo, sisi tutaendelea kujipanga sababu lazima umuheshimu mpinzania yoyote anakuja katika uwanja huu”>>>Yahya Zayd
“Ukiwa benchi Kikubwa ni kuusoma mchezo mchezaji yoyote anapokuwa kwenye benchi maana yakeni kuweza kuusoma mchezo ili akiingia akabadilishe mchez”>>>>>Yahya Zayd
Ushindi huo unaifanya Azam FC kuendelea kuwa nafasi ya pili kwa kuwa point point 36 nyuma ya Yanga wanaongoza kwa kuwa na point 38, kipigo hicho kwa Stand United kinawafanya wawe nafasi ya 15 wakiwa na point 14 ila wameizidi Azam FC na Yanga mchezo mmoja Stand United wakiwa wamecheza michezo 15 tayari ya Ligi Kuu msimu huu wa 2018/2019.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe