Kila inapofika wikendi basi mashabiki wa Soka wanajua tayari ni muda mwingine wa burudani yao wanayoipenda zaidi, Shauku ya kuwaona wachezaji wanaowapenda na kandanda la kuvutia, pamoja na kuwa kupenda Ligi mbalimbali lakini Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga huwezi kuisahau.
Jumamosi hii katika Bundesliga, Schalke 04 watakuwa nyumbani dhidi ya Borrusia Dortmund ambao wanaongoza Ligi huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote ndani ya Bundesliga tangu msimu huu ulipoanza.
Borussia Dortmund wamefunga jumla ya magoli 37 huku Schalke wakifunga magoli 14 tu katika michezo 13 ya ligi na wanashikilia nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ambayo Dortmund wanaongoza, Dortmund wanaonekana kukamilika sana katika safu ya kiungo na ushambuliaji ambayo inaongozwa na Marco Reus ambaye amaekuwa nje kwa muda akiuguza majeraha.
Reus amefunga magoli 9 na kusaidia mengine 5 huku kinara wa magoli Paco Alcacer akiwa na magoli 10 ambayo 7 kati ya hayo amefunga akitokea benchi, Utakuwa mchezo mzuri ambapo Schalke 04 wanategemea kupata matokeo katika mtanange huo wa watani maarufu kama ‘River Derby’ dhidi ya kikosi imara cha Dortmund chini ya Kocha Lucian Fevre.
Schalke 04 waliondokewa na kiungo wao tegemeo, Leon Goretzka ambaye alitimkia Bayern mwanzoni mwa Msimu huu, hawajafanya uwekezaji wakutosha kupambana na kasi ya vilabu vingine, Katika Ligi ya Ufaransa wikendi hii, mchezo wa St Etienne dhidi ya Olympique Marseille utarushwa moja kwa moja kupititia ST World Football HD sambamba na taarifa ama usimulizi wa Kiswahili.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe