Baada ya mwaka 2017 mdahalo wa wanafunzi wa vyuo vikuu Afrika kufanyika nchini Cameroon (Panafrica Universities Debates Championship), kwa mara ya kwanza katika histori ya mdahalo huo Tanzania imepewa uenyeji wa kuandaa mdahalo huo ambao umelenga kujenga uwezo wa kuzalisha viongozi na kuwajenga katika hali za kujiamini zaidi.
Tanzania ndio inakuwa nchi pekee Afrika Mashariki kuwahi kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa mdahalo huo (Panafrica Universities Debates Championship) toka uanzishwe miaka 11, ambapo mara nyingi umekuwa ukifanyikia nchi za Kusini na Magharibi.
Moja kati ya dhumuni kubwa la mdahalo wa (Panafrica Universities Debates Championship) ni kujenga na kuzalisha viongozi wa siku za usoni, kwani hivyo imetumika kama ni jukwaa la kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu vyote barani Afrika, mdahalo huo umeanza December 5 na kumalizika December 12 2018.