Usiku wa December 8 2018 ulikuwa ni usiku wa kihistoria kwa club ya Man City kwani ndio siku ambayo walikumbana na dhahama ya kufungwa kwa mara ya kwanza katika EPL baada ya kucheza game 21 mfululizo, Man City waliyokuwa Stamford Bridge kucheza dhidi ya Chelsea walipoteza game kwa magoli 2-0.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Ngolo Kante dakika ya 45 na David Luiz dakika ya 78 lakini wakati wa mchezo huo staa wa Man City Raheem Sterling wakati anaenda kuokota mpira wa kurushwa inadaiwa kuwa alifanyiwa ubaguzi wa rangi kitu ambacho Chelsea walianza kufanya uchunguzi wa haraka.
“Video imesambaa mtandaoni tutahakikisha wahusika katika video hiyo wanapatiwa adhabu, kama ikithibitika kuwa ilikuwa ni kitendo cha ubaguzi wa rangi basi mashabiki hao watafungiwa kifungo cha maisha kutoingia uwanjani kuangalia game za Chelsea” taarifa kutoka kwa msemaji
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe