Kiungo wa zamani wa Man City raia wa Ivory Coast akiitumikia Olympiakos ya Ugiriki Yaya Toure ameripotiwa kufikia maamuzi ya kuvunja mkataba na club yake ya Olympiakos, wakiwa wamekaa na kukubaliana kwa pande zote mbili.
Bado haijaelezwa kwa kina nini kimepelekea Toure na Olympiakos wafikie maamuzi ya kuvunja mkataba huo kwa makubaliano ya pande zote mbili, akiwa Toure amedumu na club hiyo kwa miezi mitatu na amepata nafasi ya kuichezea game tano toka ajiunge nayo kama mchezaji huru akimaliza mkataba wake na Man City.
Toure mwenye umri wa miaka 35 amekuwa na wakati mzuri katika maisha yake ya soka la kulipwa, akiwa amecheza soka la kiwango cha juu hadi sasa barani Ulaya kwa miaka 12, hata hivyo wakati anasaini mkataba Toure hakuweza wazi malipo yake na muda wa mkataba huo, Toure amewahi kucheza vilabu kama AS Monaco. FC Barcelona na Man City lakini aliwahi kuichezea pia Olympiakos (2005-2006).
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe