Baada ya kuwekwa benchi kwa mechi mbili mfululizo za Man United, Paul Pogba alipata nafasi ya kuanza katika mchezo wa UEFA Champions League wa kuhitimisha hatua ya Makundi kati ya Man Unitec dhidi ya Valencia, game ambayo ilimalizika kwa Man United kupoteza kwa magoli 2-1.
Kutopata nafasi ya kucheza kwa mechi mbili zilizopita na mvutano wake wa siku kadhaa na kocha wake Jose Mourinho, bado inazidisha uvumi kuwa Paul Pogba chini ya Mourinho lazima tofauti zao zitamgharimu mmoja, mchezaji wa zamani wa Man United Michael Owen ambaye ni mchambuzi wa soka kwa sasa ameeleza kuwa Pogba ni moja kati ya wachezaji bora duniani.
Owen alitoa kauli inayoashiria kuwa kocha wa Man United Jose Mourinho hajui kumtumia vizuri Paul Pogba na ndio maana anamtupia lawama lakini kama Pogba angepata nafasi ya kucheza timu anayofundisha Pep Guardiola wa Man City au Jurgen Klopp wa Liverpool basi angekuwa ni moja kati ya wachezaji bora wachache duniani.
“Nasikitishwa nikimuangalia yeye ni bora zaidi ya tunachokiona kila wiki anakuwa nje ya uwanja, kwa kiasi kikubwa nipo upande wake, sifikiri kwa namna timu inavyocheza au kocha anavyomtumia anatengeneza kupata kitu bora kutoka kwake, Kama Pogba angekuwa anacheza chini ya Guardiola au Klopp au makocha wengine wa aina hiyo basi angekuwa miongoni mwa wachezaji bora wachache duniani”>>> Michael Owen
Paul Pogba alirudi Man United kwa mara ya pili mwaka 2016 akitokea Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho inayotajwa kufikia pound Milioni 100 ila kwa miezi kadhaa sasa amedaiwa kutokuwa katika maelewano mazuri na kocha wake Jose Mourinho lakini mashabiki na wachambuzi wa soka wakimkosoa Mourinho namna avyomtumia mchezaji huyo.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe