Ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania kukidhi safari za ndani na pia kupata Watalii wengi kwa Nchi kuwa na Ndege zinazofanya safari zake moja kwa moja kutoka mataifa mengine.
Alianza kwa kununua Ndege aina ya Bombadier kisha akanunua nyingine kubwa ya Dreamliner na sasa kachukua nyingine ambapo kampuni ya kutengeneza Ndege ya Canada ya Airbus imeitambulisha Ndege hiyo mpya ambayo ni A220.
Leo Instagram Viongozi mbalimbali wamepost Msemaji wa Serikali aliandika “ya kwanza Afrika”, Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga yeye kaandika “haya sasa” na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Msigwa kaandika “Injinia soma nambaaaa a220 karibu sana”