Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu kwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, January 25,2019.
Hukumu hiyo ilitarajiwa kutolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi lakini amesema hajamaliza kuiandaa kuna vitu anavichunguza.
Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili, anadaiwa kuwa June 16, 2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa Mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.