Kocha Mkuu wa Mbao FC Amri Said akiwa ameiongoza timu hiyo kwa mechi 17 ikiwa nafasi ya nne ameamua kuondoka na kuachana na timu hiyo kutokana na kushinda kufikia makubaliano, hususani kwa uongozi kushindwa kufuata ushauri wake na mapendekezo yake.
Amri Said aliomba uongozi umuwekee kocha msaidizi lakini wao wameamua kumletea kocha Ally Bushiri ambaye wapo daraja B wote, kitu ambacho Amri Said amekuwa akihoji hapo ni nani atakuwa juu ya mwenzake, pendekezi la Amri Said ilikuwa ni kuletwa kocha wa Daraja A ili awe mkuu wake akiamini atajifunza kitu au aletwe wa daraja C ili apate msaidizi ila imekuwa tofauti.
Amri Said akiwa kaifundisha Mbao FC katika game 17 za TPL, ameshinda game 6, amefungwa game 5 na ametoka sare game 6, akifunga magoli 12 na kuruhusu kufungwa magoli 16 timu ikiwa nafasi ya 4 kwa kuwa na point 24, Amri Said alimaliza nafasi ya 6 2016/17 akiifundisha Mwadui FC na kushuka na daraja na Njombe Mji akimaliza nafasi ya pili kutoka mwisho (15) 2017/18.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe