BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, mwishoni mwa wiki ilidhamini mkutano wa kila mwezi wa chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (Tanzania Women Chamber of Commerce TWCC) mkutano ambao uliwaleta pamoja wanachama zaidi ya 250 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Akiongea wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Digitali BancABC Tanzania Silas Matoi alisema kuwa benki ya BancABC inatambua ni umuhimu wa wanawake kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na ndio sababu benki yake imeweka mikakati ya kuendelea kuwawezesha na kufikia hatua ya leo ya kuungana na Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwenye mkutano wake huu wa kila mwezi.
Matoi alisema kuwa kwenye mkutano huo BancABC imeweza kutambua kuwa wanachama wa TWCC huwa wanashiriki maonyesho mengi nchini China akitolea mfano kuwa kwa mwezi wa Oktoba na Aprili mwaka huu, wanachama 150 walishiriki baadhi ya maonyesho ya biashara nchini China. Hata hivyo, Malai alisema kuwa wakati wa safari zao nchi China wananchama hao wamekuwa wakikubana na changamoto kadhaa na hasa linapokuja suala ya kubadilisha fedha na hasa inapotokea dharura.
Ninayo furaha kuwafahamisha ya kuwa BancABC Tanzania inayo suluhiso ya jinsi ya kupata fedha za kigeni mnapokuwa safarani China. Tunayo kadi ya malipo ya kabla – YUAN pre-paid Visa card, ambayo itawawezesha kufanya malipo kwa kwa fedha za China. Kadi ya YUAN ni kadi maalum ambayo inawafanya watumiaji waweze kupata fedha za Uchina kwa thamani ile ile ambayo imewekwa kwenye kadi yake na hivyo itapunguza sana changamoto za kubadilisha fedha ambazo nyinyi wafanyabiashara huwa mnazipata pale wanapohitaji fedha za Uchina mkiwa China au popote pale duniani, alisema Matoi.
Matoi aliongeza kuwa BancABC Tanzania kwa kushirikiana na TWCC itaweza kufaidika kwa kuwa moja ya taasisi duniani ambayo imejidhatiti kutatua changamoto za wanawake na hasa kwenye masuala ya kiuchumi, kuongeza upatikanaji wa huduma na bidhaa zake, kuongeza ushirikiano pamoja na kukuza na kuongeza idadai ya wateja wake.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TWCC Mwanjuma Hamza alisema kuwa TWCC ni chama kinachounganisha wanawake kwenye sekta zote na mikoa yote, Tanzania Bara na Zanzibar.
Lengo letu ni kufanya wanawake wakue kiuchumi ikiwa ni pamoja na kukuza na kuendeleza biashara zao kwa kushiriki maonyesho kadhaa ya kibiashara ndani nan je ya nchi, alisema Hamza akiongeza kuwa kutoka Januari mpaka Disemba mwaka huu, wanawake wanachama wa TWCC walishiriki kwenye maonyesho kuanzia ngazi ya mkoa, taifa na kimataifa na hivyo kuwajengea uwezo wa kukuza biashara zao kutoka na ujuzi wanaoupata.
Akifafanua zaidi, Hamza alisema wanawake wananchama wa TWCC 150 walishiriki maonyesho nchini China, 100 Ujerumani na kwa sasa kuna wanawake wapatao 30 ambao wanaendelea na maonyesho Eldoret, Kenya.
Rais Magufuli amtumia Mstaafu Mkapa salamu za rambirambi