Meneja wa Uwanja wa ndege Mwanza Maulid Mohamed amesema ni kweli kulikuwa na taarifa ya ajali ya ndege ila kiuhalisia sio ajali kwani yalikuwa ni mazoezi ya namna ya uokoaji kwenye usafiri wa anga.
“Ndege ilikuwa inapita kutoka Kigali kwenda Nairobi rubani akatangaza ndege yake ina tatizo la injini wakati anajaribu kutua ikapata ajali” Meneja Airport
“Ndege hiyo aina ya Boeing 737 ilikuwa na abiria 45, Marubani 2, na Wafanyakazi 3, kimsingi hakukuwa na mtu swala la kupoteza maisha halikuwepo” Meneja Airport Mwanza
“Hatukuwapa taarifa ukiwapa taarifa huwezi kuwapima na huwa tunafanya kila baada ya miaka miwili, tuombe radhi kama imetokea kumpa shida mtu yeyote” Meneja Airport Mwanza