Kiungo wa Armenia mwenye umri wa miaka 29 anayecheza club ya Arsenal Henrikh Makhitaryan kupitia websites rasmi ya club yake, imetangaza kuwa itamkosa mchezaji huyo kufuatia kubainika kuwa amevunjika mfupa mdogo wa mguu wake unaoungana na vidole vya mguu.
Henrikh alibainika kuumia baada ya kucheza game ya Carabao Cup dhidi ya Tottenham Hotspurs kwa dakika 45 na kutolewa nje, hiyo ni kabla ya kufanyiwa uchunguzi wakiwa na madaktari, hivyo Mkhitaryan ataanza mazoezi mepesi mepesi na timu yake baada ya wiki sita ndio kocha aanze kumtumia tena katika mechi za ushindani.
Hata hivyo baada ya Mkhitaryan kushindwa kumaliza game dhidi ya Spurs iliyomalizika kwa Arsenal kupoteza kwa magoli 2-0, alikosekana pia katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Burnley uliyomalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa magoli 3-1, Arsenal kwa sasa inapambania kumaliza TOP 4 katika EPL baada ya kuwa nafasi ya tano kwa muda sasa.
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati