Moja kati ya habari kubwa duniani katika soka leo ni habari ya beki wa kati wa Napoli Kalidou Koulibaly kuingia katika headlines kufuatia kubaguliwa na mashabiki wa Inter Milan wakati wa game dhidi yao, game ambayo Inter Milan alikuwa nyumbani.
Leo mastaa mbalimbali wa soka duniani wameoneshwa kuguswa na kusikitishwa na kitendo cha mashabiki wa Inter Milan kuonesha kitendo cha ubaguzi wa rangi kwa Kalidou Koulibaly, kufuatia kitendo hicho kilichotokea wakati wa mchezo huo, Inter Milan sasa wameadhibiwa kwa kufungiwa game zao mbili za nymbani kucheza bila mashabiki.
Ubaguzi wa rangi kitendo ambacho kinapingwa kwa kiasi kikubwa katika michezo hivyo, shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kupitia nchi wanachama wake wamekuwa na utamaduni wa kukemea vitendo hivyo, kufuatia dalili za kubaguliwa kwa Koulibaly kocha wa Napoli Carlo Ancelotti aliomba karibia mara tatu game hiyo iahirishwe.
Game tatu zijazo za Inter Milan za nyumbani ni Sassuolo 19 January, Bologna 3 February na Sampdoria 17 February, kwa upande wa Koulibaly, Serie A wamemfungia game mbili kutokana na game hiyo kuoneshwa kadi nyekundu, game hiyo ilimalizika kwa Napoli kupoteza kwa 1-0.
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati