December 30, 2018 Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko pamoja na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde wamefanya ziara ya kushtukiza katika viwanda vya kuzalisha kokoto vya kampuni ya Laroy Agregates na WADI mkoani Dodoma ambazo zinafanya kazi ya kupeleka kokoto katika ujenzi wa mji wa Serikali Ihumwa.
Naibu Waziri Biteko ametoa siku nne kwa wahusika kurudi kazini baada ya kudaiwa kusitisha kazi za uzalishaji na kwenda likizo.
MWANZO MWISHO: MAMA ASIMULIA MWANAE MCHANGA ALIVYOFUNGIWA KABATINI NA BOSI WAKE