Club ya Yanga SC usiku wa January 7 2019 imeyaaga rasmi mashindano ya Mapinduzi Cup 2019 baada ya kupokea kipigo cha pili katika michuano hiyo, Yanga ilikuwa inacheza dhidi ya Malindi SC katika uwanja wa Amaan Zanzibar, hiyo ikiwa ni game yake ya tatu Kundi B.
Yanga ambao kikosi chao cha kwanza wamekiacha Dar es Salaam kwa ajili ya michezo ya Ligi Kuu na kuleta Zanzibar kikosi cha team B na wachezaji baadhi wakikosi cha kwanza, wamejikuta wakipokea kipigo cha magoli 2-1 na kuyaaga mashindano hayo, magoli ya Malindi yalifungwa na Abdulswamadu dakika ya 42 na Juma Boluna dakika ya 62 huku goli pekee la Yanga likifungwa mapema dakika ya 35 na Matheo Anthony.
Kwa matokeo hayo Yanga akiwa Kundi B lenye timu za Azam FC, KVZ, Jamhuri na Malindi sasa anaaga mashindano akiwa kabakiza mchezo mmoja wa kukamilisha ratiba dhidi ya Jamhuri siku ya Jumatano ya January 9 2019.
Kundi B linaongozwa na Azam FC wakiwa na point 7, wakifuatiwa na Malindi SC wenye point 7, Jamhuri wana point 4 hivyo Yanga waliopo nafasi ya mwisho wanacheza game yao ya kumalilisha ratiba kwani hata wakishinda game ya mwisho watakuwa na point 6 ambazo haziwezi kuwaweka nafasi mbili za juu na kucheza nusu fainali.
Mbona Jonas Mkude hatumuoni Zenji? Meneja wa Simba kajibu