Tume ya Uchaguzi nchini DRC imetangaza matokeo ya uchaguzi wa Urais uliofanyika December 30, 2018 nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo ambapo Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi Tshilombo ameibuka mshindi katika uchaguzi huo akipata asilimia 38.57 ya kura, kwa mujibu wa CENI.
Matokeo ya awali yanaonyesha Mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na Mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na Serikali Emmanuel Shadary.
Tshisekedi amepata zaidi ya kura Milioni 7 nae Fayulu amepata kura takriban Milioni 6.4 milioni, huku Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura Milioni 4.4.
Matokeo kamili yanatarajiwa kutangazwa January 15 na Rais mpya ataapishwa siku tatu baadaye, kulinagana na ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI).
Felix Tshisekedi ni Mtoto wa mwanzilishi wa Chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), Mwanasiasa wa Upinzani wa muda mrefu nchini DRC Etienne Tshisekedi.
Baba yake alifariki February 2018 na sasa Mwanawe anatarajia kutumia msingi wa umaarufu wa baba yake katika kipindi hiki.
Kama matokeo yatathibitishwa, Tshisekedi atakuwa Rais nae Kamerhe, ambaye ni Rais wa zamani wa Bunge na ambaye aliwania dhidi ya Kabila mwaka 2011 atakuwa Waziri Mkuu.
Tshisekedi atakuwa Mgombea wa kwanza kabisa wa upinzani kushinda uchaguzi wa Urais tangu DRC ilipojipatia uhuru.
Via RFI Swahili
BREAKING: AJALI YA TRENI NA SCANIA IMETOKEA DODOMA, INADAIWA KUNA VIFO