January 10 2019 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Hamza Johari amezindua mnara mpya kwa ajili ya uongozaji wa Ndege katika Kiwanja cha Ndege Pemba
Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Milioni 300 ni miongoni mwa miradi iliyozinduliwa katika wiki ya Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mradi huo umegharimiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.
Ukarabati umefanywa na Kampuni ya Kitanzania ya M/s Future Century Limited ambapo kazi zilizofanyika ni pamoja na kubadilisha vioo vinavyozunguka mnara wa kuongozea ndege, kurekebisha paa na kuzuia kuvuja, kuweka vizuizi vya usalama (guard rails) na kuweka upya mfumo wa viyoyozi (Air conditioning), kuweka upya mfumo wa umeme, kuweka upya mfumo wa simu na taarifa za kieleckroniki na kupaka rangi upya.