Leo January 15, 2018 Benki kuu ya Tanzania imehamisha madeni na mali zote za Bank M kwenda Azania Bank kutokana na Benki hiyo kushindwa kujiendesha Wateja wenye mikopo wametakiwa kuendelea kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Naibu Gavana amesema “Kwa Mamlaka iliyopewa BOT kwa mchakato wa kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M umekamilika, Benki Kuu imeamua kuwa mali na madeni ya Bank M yatachukuliwa na Benki nyingine kama njia ya ufumbuzi wa matatizo ya Bank M”
“Mali na madeni ya Bank M yanaenda Azania Bank, kwa sasa Benki Kuu na Azania Bank wanaendelea kuandaa taratibu za Kisheria za kukamilisha mchakato wa uhamishaji wa mali na madeni ya Bank M kwenda Azania Bank Limited” Naibu Gavana BOT
MAAJABU: GENGE LINALOJIUZA, UNALIPA HELA UNACHUKUA CHENCHI MWENYEWE