Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya DSM, amekataa kupokea shauri la Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe la kutaka tafsiri ya Katiba na Sheria Kuhusu mamlaka ya Spika wa Bunge kumwita na kumshtaki Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama, Rais wa TLS, Fatma Karume akiwa na Zitto Kabwe amesema Msajili amewapa sababu mbili za kukataa kesi yao.
Karume amesema kuwa sababu hizo ni kwamba katika hati ya kiapo Zitto hajaambatanisha wito wa Spika wa Bunge kwenda kwa CAG.
Pia amewataka warekebishe majina ya walalamikaji ambapo waliyaondoa na kubaki jin moja la Zitto Kabwe.
“Suala la kiapo ni ushahidi na sio kazi ya msajili bali ni kazi ya Jaji na hati ya kiapo aliyoitoa Zitto lazima ajibiwe,
“Kinachotekea hapa mahakama inaamua kesi kabla ya kusikilizwa ni kitu cha kuudhunisha sana kwani mahakama inapofikia hapa bila kusikiliza pande zote mbili imekuwa ni siku ya kuudhunisha,” Fatma Karume
Kutokana na hatua hiyo, Fatma Karume na Zitto wamewasilisha malalamiko yao kwa Jaji Mkuu wa Tanzania kuhusu suala hilo.
INASIKITISHA: MWILI UMEOKOTWA MTARONI UKIWA NDANI YA KIROBA