Leo January 16, 2019 tunayo story kutokea Soko la Kimataifa la Samaki Feri jijini Dar es Salaam, ambapo wavuvi katika soko hilo wamezungumzia kadhia ya kukamatwa kwa vyombo vyao vya uvuvi kwa sababu ya kutokuwa na leseni za mwaka 2019.
Akizungumza kuhusu kadhia hiyo, Mwenyekiti wa wavuvi soko la Feri, Salehe Msiani amesema hatua hiyo imesababisha shughuli za uvuvi zisimame kwa siku ya jana na juzi kutokana na wavuvi wengi kuhofia kukamatwa.
Amesema kukamatwa kwa wavuvi hao na vyombo vyao kundaiwa ni kutokuwa na leseni za mwaka 2019, licha ya kuwa muda wa kukata bado wanao.
“Hakuna anayepinga hiyo sheria isipokuwa muda wa kukata leseni bado upo, lakini kwa sababu wavuvi wanakamatwa wanaohofia kuwasha vyombo na kuingia majini, ndio maana jana na juzi samaki hawakuuzwa,”amesema.