Uamuzi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake kuamua kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20 na asilimia 10 kwa Mawaziri wake, ulipokelewa kwa mitazamo tofauti ya watu mbalimbali huku wengi wakionyesha kuunga mkono.
Sasa jingine jipya kwa sasa ni kuhusu Rais Uhuru kuagiza wakuu wote wa mashirika ya serikali nchini Kenya kupunguzwa mshahara kwa asilimia 20 na kwamba watakaopuuza agizo hilo watafutwa kazi ili nafasi hizo wapewe wengine walio tayari kupokea mshahara wa chini.
Namkariri akisema ‘Nakuhakikishia kuna Wakenya wengi wako tayari kuchukua hizo nafasi kwa mshahara huohuo mdogo, watakaogoma kupunguzwa mshahara waondoke waende Mahakamani ambako hata wakishinda itakua rahisi sisi kulipa fidia na kupata watu wengine hivyo wasidhani wataturudisha nyumba kwa kwenda Mahakamani’
‘Kama huwezi kukubali nenda utafute pahali ambapo wako tayari kukulipa huo mshahara na hiki ni kitu ambacho kitaendelea kufanyika kwenye sehemu zote, na niwakumbushe tu kwamba hatufanyi hivi kwa ajili ya kumuumiza yeyote’ – Uhuru Kenyatta
Wakati huohuo Chama cha ODM kimepinga vikali hili agizo la Rais Kenyatta la kulazimisha wafanyakazi wa Serikali kukubali mshahara wao kupunguzwa na kwamba Rais na Naibu wake ni wanafiki.
ODM wanasema wawili hawa hawana majukumu ya kulipa kodi ya nyumba au nauli miongoni mwa majukumu mengine huku marupurupu wanayopokea yakiwa makubwa bado hivyo kukatwa asilimia 20 ya mshahara wao haitosaidia kuboresha maisha ya Wananchi.
Hii ishu umeionaje?