Muigizaji Martina Big ’31’ kutokea Ujerumani ameamua kujibadilisha ngozi yake na kuwa ya Kiafrika baada ya kuchomwa sindano zinazoaminika kuwa zitambadilisha kuwa mweusi pamoja na kuzaa watoto wenye rangi ya Kiafrika.
Inaripotiwa kuwa Martina Big pamoja na mume wake Michael ambaye ni rubani wa ndege walichukua maamuzi hayo January,2017 na kuamini kuwa wakifanya hivyo watapata watoto chotara, huku ikitajwa kuwa kwa miaka kadhaa Martina alianza kujibadilisha nywele na kutaka ziwe ngumu na baadae alijibadilisha sura.
Mwaka 2018 Martina Big alisafiri na kulekea Nairobi Kenya ambapo alibatizwa na kuitwa ‘Malaika Kubwa’ na kutangazwa kuwa mwanamke halisi wa Kiafrika. Pia Martina alipata umaarufu mkubwa baada ya kufanya upasuaji mara 23 wa kujiongeza matiti ili yawe makubwa.
SIMULIZI : UGONJWA WA ‘LUPUS’ UNANIMALIZA NILIFUKUZWA SHULE