Mshambuliaji wa kiargentina Gonzalo Higuan usiku wa January 23 2019 alitangazwa rasmi kujiunga na club ya Chelsea iliyochini ya kocha Maurizio Sarri kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita akitokea Juventus ya Italia, hiyo ni baada ya kudumu kwa muda mfupu kwa mkopo akiwa AC Milan.
Hata hivyo Higuan yupo kwa mkopo Chelsea katika mkataba ambao wanaweza kumnunua mwisho wa msimu kwa pound milioni 31.3 au kumuongezea mkataba wa mkopo na kumlipa pound milioni 15.6 katika miezi 12 ili kujihakikisha kupata huduma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.
Higuan akiwa na AC Milan kwa mkopo wa muda mfupi msimu huu amecheza michezo 22 na kufunga magoli nane ila alikuwa na wakati mzuri na kufunga zaidi msimu wa 2015-2016 akiwa Napoli chini ya kocha Maurizio Sarri, kitu amabacho alifanya kuifikia rekodi ya ufungaji wa muda wote Serie A akiwa na magoli 36 kwa msimu na kuifanya Juventus kutoa pound milioni 75 kumsajili akitokea Real Madrid.
“Maurizio Sarri ni kocha ambayo katika maisha yangu ya soka amepata kuuona ubora wangu na anajua namna ya kufanya kazi na mimi, ule mwaka tuliokuwa pamoja ulikuwa wa bora sana na namshukuru kwa hili, hivyo kurudi kufanya kazi pamoja ni kitu muhimu kwangu, Nina furaha kupewa hii fursa tena ila ule mwaka ulikuwa mzuri na kuvunja rekodi kwangu ilikuwa muhimu sana”>>> Higuan
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”