Kikosi cha Simba SC jioni ya leo January 29 kimesafiri kuelekea Alexandria Misri kwa ajili ya mchezo wake wa tatu wa CAF Champions League Kundi D dhidi ya Al Ahly, wakiwa wanaelekea safari hiyo Haruna Niyonzima amefunguka na kujibu tuhuma za kudaiwa wachezaji saba wa Simba akiwemo yeye walitoroka kambini.
Niyonzima amefika mbali zaidi na kumtetea mchezaji mwenzake Pascal Wawa kutokana na video clip ilyokuwa imesambaa ikimuonesha anacheza muziki na mwanamke, hivyo video hiyo ikaanza kuhusishwa kuwa ni video ya siku aliyotoroka kambini.
“Watu wametafsiri tofauti naweza kusema hivyo sisi kama wachezaji tunajua hakuna kitu cha hatari kilichotokea, hatujaonekana labda kama video unayo wewe lakini mimi sijaiona, unajua ile video ya Wawa mimi sio kwamba namtetea ni video ya muda sio ya siku hiyo isipokuwa sisi binadamu tatizo dogo likitokea watu wanaleta na vitu ambavyo vilikuwa havihusiki”>>>Niyonzima
STEVE NYERERE AIBUKA KWA MANARA: ”MUACHE AJIPONGEZE KWA KIPIGO”