Watu wawili wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili aina ya Scania na Ashok kugongana uso kwa uso kisha kuwaka moto katika eneo la Makunganya nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Kamishina msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Polisi, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa moja lilikuwa linatokea maeneo ya Dodoma kuelekea Morogoro na jingine lenye namba za usajili T6616 DKS lilikuwa linatokea Morogoro kwenda Kagera.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Lyamuya amesema wamepokea majeruhi hospitalini hapo na wananendelea kupatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.