Leo January 31, 2019 Hiki ndicho alichoandika Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema katika ukurasa wake wa Twitter akijibu kile kilichosemwa Bungeni Dodoma kumhusu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
“Bunge halijawahi kumlipia Lissu pesa kwa ajili ya matibabu alichokisema Spika Ndugai ni upotoshaji kwa jamii na Mungu. Chama kitatoa tamko juu ya hili. Spika akiweza kuthibitisha hili, Mimi nitajiuzulu Ubunge, mshahara wa Mbunge sio hisani ya Spika” Lema
SPIKA NDUGAI “TUMEMLIPA TUNDU LISSU MILIONI 25O, AKIKANUSHA NATOA MKEKA”