Baada ya kucheza mchezo wao wa kwanza nyumbani wa hatua ya Makundi wa CAF Champions League, Simba SC ilifuata kwa kucheza michezo yao ya pili ya michuano ugenini, baada ya kupoteza 5-0 dhidi ya AS Vita katika jiji la Kinshasa DRC, Simba leo ilikuwa Alexandria Misri kukipiga dhidi ya Al Ahly.
Simba ambao walikuwa na jeraha la kupoteza kwa magoli 5-0 mchezo wao wa AS Vita, wamejikuta wakiingia kwenye aibu nyingine tena baada ya kujikuta wakipokea kipigo kingine cha magoli 5-0, huku Al Ahly ikimkosa nyota wake Ramadan Sobhi kwa majeraha.
Dakika 45 za kwanza wamejikuta Simba wakiwa wameruhusu tayari magoli 5-0, hivyo baada ya kuongeza nidhamu ya ulinzi kipindi cha pili, walifanikiwa kuzuia na kutoongezwa goli lolote, kipigo hicho kinaifanya Simba iendele kuwa nafasi ya tatu kwa kuwa na point 3, JS Saoura akishika mkia kwa kuwa na point 4.
Magoli ya Al Ahly yalifungwa na Sulaya dakika ya 3, Maaloul dakika ya 23, Ajayi dakika ya 31 na Walid aliyefunga magoli mawili dakika ya 34 na 40, baada ya game hiyo Simba sasa watacheza game yao ya nne nyumbani dhidi ya hao hao Al Ahly February 12 2019 uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF