Moja kati ya stori inayotrend kwa sasa katika soka bongo ni kuhusiana na club ya Simba SC kufungwa 5-0 dhidi ya Al Ahly katika mchezo wao wa tatu wa hatua ya makundi wa CAF Champions League, baada ya kipigo hicho msanii wa Bongofleva Afande Sele ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe mzito kuhusu ishu za ujanja ujanja Simba SC.
“Wakati ule wanasimba wanafurahia ujio wa Mo wakiamini kwamba timu itakua bora kwa sababu itakua na mahela ya udhamini sisi wengine tulikaa kimya tukisubiri kuona hayo mabadiliko ya uendeshaji wa timu atakaokuja nao Mo ambayo tulitegemea angeitoa Simba ktk uendeshwaji wa kikariakoo uliozoeleka na kuiendesha kitaalamu kama inavyotakiwa lakini kumbe Mweh”
“Udhamini wa Mo simba umefanana na shehe aliyebadilisha kanzu wkt yeye ni yuleyule kwa sababu pamoja na udhamini wa Mo Simba imeendelea kuendeshwa kienyeji na kisanii tu hadi wkt mwingine mtu timamu unajiuliza hivi huyu ni Mo yuleyule mdau mkubwa wa soka la bongo anaelijua nje na ndani au huyu ni Mo mpya na mgeni kabisa wa soka letu?”
“Chini ya udhamini mnono wa Mo lkn Simba imeendelea kuwatumia madalali wapiga dili walewale ktk usajili wa wachezaji hadi benchi la ufundi..Simba pamoja na udhamini wa Mo lkn bado inasajili wachezaji magarasa kutoka nje ya nchi ambao hata timu zao za taifa haziwajui kabisaaa na matokeo yake wanachukua wachezaji wa kuja kujaribiwa badala ya kuja kucheza”
“Mfano ktk hao mapro wa Simba ukimtoa Kagere na Chama ni nani mwingine anaechezea timu yake ya taifa?…hii maana yake ni kwamba ktk kusaka wachezaji Simba chini ya Mo bado inawatumia wapiga dili walewale wa miaka yote ambao wao wanaangalia ten percent yao tu wala sio kuisaidia Simba na soka la Bongo kiujumla”
“Nakumbuka baada ya Simba kutobolewa tundu na Kagera sugar mbele ya Rais Jpm huyu mzee aliongea kiroho safi tu kwamba kwa wachezaji na uchezaji ule Simba inakwenda kutia aibu ktk mashindano ya kimataifa labda ifanye usajili mkubwa wenye tija kitu ambacho bila shaka viongozi wa Simba na mdhamini wao walichukulia poa tu na sasa wanavuna uvivu wao wa kutochukua hatua stahiki”
“Maajabu ya dunia ambayo yanapatikana Simba pekee ni vile et msemaji wa timu ananguvu na ushawishi mkubwa kuliko hata benchi la ufundi na kisa anajua maneno ya kumpamba bosi mkuu kiasi cha yule boss kuona misifa anayopewa na huyo msemaji ni sawa na pafyumu..hahahaaaaa..et Simba inakikosi kipana hivyo size yetu ni Barcelona,Madrid,Arsenal,Man U nk…full maneno ya khanga half viongozi,wanachama na mdhamini wanachekelea kama majuha tu matokeo yake ndio haya 5+5”
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF