Taarifa kutoka Mjengoni (104.4 Clouds Fm) hatimae Samuel Sitta ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge la katiba kwa kupata jumla ya kura 487 kati ya kura zote 563 zilizopigwa na wawakilishi wa bunge hilo,na kwa sasa Samuel Sita anatoa hotuba yake ya shukrani kama Mwenyekiti.
Miongoni mwa changamoto alizoziahidi kuzishughulikia ni pamoja kulifanya bunge hili kuwa bunge la viwango na kuahidi kutumia muda mfupi zaidi kwenye bunge hili la Katiba sambamba na kuwashughulikia wanaotaka muungano uvunjike.
Samuel John Sitta amewahi kuwa Spika wa Bunge la tisa na sasa ndiye Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba baada ya kushinda kwa kura 487 dhidi ya 69 alizopata mpinzani wake ambae ni Hashim Rungwe.
Kesho March 13 zitapigwa kura kumtafuta Makamo Mwenyekiti wa Bunge hili ambapo kulingana na sababu za kimuungano atatokea upande wa Tanzania visiwani(Zanzibar) na kuweka usawa wa jinsia kwa hivyo atakaechaguliwa kutoka huko atakuwa ni Mwanamke.