Dkt Anthony Mwandulami ambaye ni Mganga wa tiba asilia anaeishi Mkoa wa Njombe Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ameshaanza kujijengea kaburi lake tayari lenye thamani ya Bilioni 1 ili akifariki azikwe yeye na Wake zake watatu.
Akizungumza na AyoTV Mwandulami amesema kwamba sababu kuu inayomfanya kujijengea kaburi hilo ni kuhifadhi historia yake baada ya kifo, “Kaburi hili si tu limeleta mshangao kwa wakazi wa eneo la Njombe, lakini pia linawashtua wengi nchini kote”.