February 7 2019 zimetolewa good news kuhusiana na nafasi za utawala katika shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kuelekea uchaguzi wa shirikisho hilo, FIFA ilikuwa imepanga kufanya uchaguzi mkuu wa FIFA June 5 lakini baada ya kutotokea kwa mpinzani ni wazi Gianni Infantino ataendelea.
Rais wa sasa wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Gianni Infantino kutokana na kukosa mpinzania wa kugombea nafasi yake ataendelea kutawala kama Rais wa FIFA hadi mwaka 2023 ambpo atakuwa anamaliza muhula wa pili wa utawala.
Ili Rais Infantino apate wapinzani ni lazima mashikirikisho au nchi wanachama wa FIFA watano watoe wagombe kitu ambacho hakijatokea, hivyo hiyo inamaanisha FIFA uongozi uliopo ambao unapata sapoti kutoka mashirikisho 190 utaendelea kuwa madarakani.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF