Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 imeendelea leo kwa game mbili kupigwa ila Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Simba SC walikuwa wenyeji wa Mwadui FC uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba ambao wanakabiliwa na game yao ya CAF Champions League dhidi ya Al Ahly February 12 walitumia kikosi chao kamili katika mchezo huo.
Simba SC ambao ndio timu inayoongoza kuwa na viporo vingi katika Ligi Kuu ukilinganisha na zingine kutokana na ushiriki wake katika michuano ya CAF Champions League, leo imecheza game ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 kwa mara ya kwanza baada ya siku 40 kupita kutokana na michezo yake kuahirishwa ili kuwapa nafasi ya kucheza game za CAF Champions League.
Leo Simba SC ikiwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao ndio inautumia kama uwanja wake wa nyumbani, ilifanikiwa kuifunga Mwadui FC kwa magoli 3-0, magoli ya Simba yakifungwa na Meddie Kagere dakika ya 21, Mzamiru Yassin dakika ya 25 na John Raphael Bocco nahodha wa timu hiyo akafunga goli la mwisho dakika ya 29, Simba ni sawa na kusema imechukua point tatu kwa kufunga magoli matatu ndani ya dakika 9.
Simba sasa baada ya ushindi huo inaendelea kuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa inajumla ya point 36 ila imezidiwa michezo saba na Yanga SC wanaoongoza Ligi ikiwa na point 55 kwa kucheza michezo 22, Azam FC ikiwa nafasi ya pili kwa kuizidi Simba SC michezo sita na kuwa na point 48 wakicheza michez0 21 Simba wakiwa wamecheza michezo 15 pekee, Mwadui wanaendelea kuwa nafasi ya 16 kwa kuwa na point 24 wakicheza game 25.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF