Moja kati ya habari kubwa katika soka la bongo ni pamoja na ishu ya mchezaji wa Stand United Harerimana Moussa Hafizi kudaiwa kucheza Ligi Kuu soka Tanzania bara akitambulika kama mchezaji wa kitanzania wakati huyo ni mchezaji wa Burundi na hata timu ya taifa amewahi kucheza ya nchi hiyo.
Kubwa lililofanya stori hiyo kubwa sio Harerimana kucheza soka Tanzania ila kucheza Ligi Kuu kwa madai ya kinyume na taratibu huku akitambulika kama mchezaji wa Tanzania, hivyo anacheza Tanzania pasipo kuwepo na ITC au nyaraka ya kumtambua yeye ni mchezaji wa kigeni.
Mbunge wa Manonga Seif Gulamali ameiibua tena ishu hiyo na kudai majibu kutoka TFF baada ya kuona hadi leo TFF, ambao ndio wasimamizi na waendeshaji wa Ligi hiyo kukaa kimya pasipo kutolea ufafanuzi wowote kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Harerimana, Gulamali ameandika hivi kutumia ukurasa wake wa instagram
“Hii Ishu TFF kama wameamua Kukaa Kimya na kuipotezea lakini wajue tunafuatilia Nyendo zao.Mchezaji wa Stand Utd mwenye Uraia wa Burundi lakini hana Leseni ya kucheza Tanzania na Stand wamemtumia katika Mechi Nyingi tu”>>> Seif Gulamali
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF