Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliopata nafasi ya kuhudhuria mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba SC kupata ushindi wa goli la dakika ya 71 lilofungwa na Meddie Kagere na kuufanya mchezo kumalizika 1-0.
Dr Mwakyembe amezichukua headlines kwa kitendo chake cha kutotaka kujulikana yeye ni shabiki wa timu gani zaidi kati ya Simba na Yanga na ndio maana akaamua kwenda Taifa akiwa kashona shati lilokuwa na rangi tano ambazo ni nyekundu, nyeupe ambazo zinatumiwa na Simba na nyeusi, njano na kijani ambazo zinatumiwa na Yanga.
Kwenda uwanjani akiwa kavaa shati lenye rangi hizo wengi wametafsiri kama ni kitendo cha waziri kutotaka kufungamana au kuonekana yeye ni shabiki wa timu gani, hii sio mara ya kwanza kwa waziri wa michezo kwenda kushuhudia game za Simba na Yanga akiwa na shati la namna hiyo, iliwahi kutokea mwaka 2012 katika fainali ya Kagame Cup ambapo Dr Emanuel Nchimbi alienda kavaa shati lenye rangi mbili njano na nyekundu.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba