Baada ya Bodi ya Filamu Tanzania leo Feb 18 2019 kumfungulia adhabu iliyotokana na kufungiwa kutofanya shughuli za filamu kwa muda usiojulikana Muigizaji Wema Sepetu kutokana na video yake ya kimahaba kusambaa kwenye mitandao ya kijamii October 26 2018, Muigizaji huyo amezungumza haya.
”Nadhani kwamba mnajua ni jinsi gani ninavyopenda kazi yangu, naipenda, naihusudu, naithamini, kwa hiyo mtegemee vitu vingi sana, vipya kutoka kwangu, vizuri na naahidi Watanzania kwamba sitawaangusha” Wema Sepetu