Tanzania imeanzisha mfumo wa anwani mpya za kitaifa na postikodi ambao ni mfumo maalum wa
alama, tarakimu na herufi inayotambulisha eneo au mahali mtu anapoishi au kufanyia shughuli zake.
Kama sehemu ya utekelezaji wa mfumo huu, makazi ya watu yanapewa namba ili kutambulika na kufikiwa kwa urahisi.
Nakuwekea baadhi ya faida za mfumo huu ni:
1. Kurahisisha kufikiwa kwa maeneo mengi kwa ajili ya huduma mbalimbali.
2. Kuwezesha kupanga na kusimamia mipango mahsusi ya kutoa huduma kwa wananchi.
3. Kurahisisha utoaji wa huduma za dharura kama vile uokoaji na kukabiliana na maafa.
4. Kuongeza ufanisi katika usimamizi wa makazi ya watu.
5. Kurahisisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kwa makusudi mbali mbali.
6. Kuimarisha utawala bora
Majibu ya Sengo baada ya kubananishwa ishu ya kuzaa na Steve