Kijana Musa Yahya anayeisha Namanga Wilayani Longido Mkoani Arusha amefika mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola kumlalamikia jinsi alivyopigwa na Askari kwa siku 14 katika Tarafa ya Loliondo hadi kupeleka mguu wake kuoza akiwa katika kituo cha Polisi kwa madai ya kuwaibia Wazungu.
Akizungumza mbele ya Waziri Lugola amedai kwamba alipigwa nakuingiziwa chupa sehemu za siri. Baada ya malalamiko hayo Waziri amesema baadhi ya Askari wamekuwa wakiharibu taswira ya Jeshi la Polisi nakusema haki itatendeka na kila mmoja atabeba mzigo wake.